Wednesday, May 16, 2012

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA)kimeendeleza kampeini yake ya kuhamasisha wananchi kukiunga mkono katika jimbo la Muleba kusini,na kufanikiwa kupata jumla ya wanachama wapya 112 katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa red cross mjini Muleba jana jioni.

Shamrashamra hizo za CHADEMA zilitanguliwa na ufunguzi wa ofisi ya chama ya jimbo la Muleba kusini lililoko wilayani Muleba,jimbo ambali kwa sasa linashikiliwa na mbunge wa CCM ambaye pia ni waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Kajumulo Tibaijuka.

Mkutano huo uliokuwa umemkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Kagera Wilfred Rwakatare,ulihudhuriwa na wananchi wengi kutoka sehemu mbalimbali ndani ya mkoa wa Kagera pamoja na kuhudhuriwa na mbunge wa viti maalumu Chadema Conchesta Rwamulaza,Anna Mukono ambaye ni Mwenyekiti wa baraza la wanawake wa chadema mkoani hapa pamoja na madiwani mbalimbali kutoka vyamma vingine vya upinzani vilivyo ndani ya wilaya ya Muleba.

Katika mkutano huo,chama hicho kiliweza kuvuna idadi ya wanachama wapya ndani ya chama hicho 112,huku wanachama 45 walirudisha kadi kutoka vyama vingine vya siasa na wanachama 67 walijiunga kwa kununua kadi na kujisajili upya.

Baadhi ya wanachama walioweza kujiunga chama hicho kwa kurudisha kadi ni 21 kutoka CCM,wanachama 11 kutoka TLP,wanachama 7 kutoka CUF na wanachama 6 kutoka NCCR Mageuzi.

Aidha,chama hicho kiliendesha harambee ili kupata mchango wa kuweza kuendesha ofisi jimboni hapo,ambapo harambee hiyo iliendeshwa na diwani wa kata ya Buseresere wilayani Chato mkoani Geita Sprian Kagoma na kufanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi 485,000/=ikiwa ni fedha taslimu.

CHADEMA WAVAMIA JIMBONI KWA PROF.TIBAIJUKA.......WAVUNA 112!

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA)kimeendeleza kampeini yake ya kuhamasisha wananchi kukiunga mkono katika jimbo la Muleba kusini,na kufanikiwa kupata jumla ya wanachama wapya 112 katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa red cross mjini Muleba jana jioni.


Shamrashamra hizo za CHADEMA zilitanguliwa na ufunguzi wa ofisi ya chama ya jimbo la Muleba kusini lililoko wilayani Muleba,jimbo ambali kwa sasa linashikiliwa na mbunge wa CCM ambaye pia ni waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Kajumulo Tibaijuka.

Mkutano huo uliokuwa umemkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Kagera Wilfred Rwakatare,ulihudhuriwa na wananchi wengi kutoka sehemu mbalimbali ndani ya mkoa wa Kagera pamoja na kuhudhuriwa na mbunge wa viti maalumu Chadema Conchesta Rwamulaza,Anna Mukono ambaye ni Mwenyekiti wa baraza la wanawake wa chadema mkoani hapa pamoja na madiwani mbalimbali kutoka vyamma vingine vya upinzani vilivyo ndani ya wilaya ya Muleba.

Katika mkutano huo,chama hicho kiliweza kuvuna idadi ya wanachama wapya ndani ya chama hicho 112,huku wanachama 45 walirudisha kadi kutoka vyama vingine vya siasa na wanachama 67 walijiunga kwa kununua kadi na kujisajili upya.

Baadhi ya wanachama walioweza kujiunga chama hicho kwa kurudisha kadi ni 21 kutoka CCM,wanachama 11 kutoka TLP,wanachama 7 kutoka CUF na wanachama 6 kutoka NCCR Mageuzi.

Aidha,chama hicho kiliendesha harambee ili kupata mchango wa kuweza kuendesha ofisi jimboni hapo,ambapo harambee hiyo iliendeshwa na diwani wa kata ya Buseresere wilayani Chato mkoani Geita Sprian Kagoma na kufanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi 485,000/=ikiwa ni fedha taslimu.

Tuesday, May 15, 2012

VACADO SOKONI

WAKULIMA mkoani Kagera tubadilike kwa kilimo cha mazoea,tujikite katika kilimo cha biashara zaidi.


VACADO ni zao mbadala la kiashara ambapo kila kukicha thamani yake inapanda kutokana na mahitaji yake.Ni zao ambalo halihitaji mbolea kama yalivyo baadhi ya mazao mengine,linauzika kwa kiwango kikubwa katika masoko mengi hapa nchini,mathalani katika soko la Bukoba kila Vacado moja linanunuliwa kati ya shilingi 350 hadi 500.


Miche ya zao hili inapatikana kwa urahisi mno,hasa wilayani Muleba kwa bw.Novatus Kashaga,mkulima wa kijiji Itoju kata Izigo.Mkulima huyu tayari ana kitaru cha miche mia hamsini elfu(150000)yuko tayari kuuzia kila atayehitaji kulima zao hili ili kupunguza wimbi la umasikini.

Sunday, May 13, 2012

MADEREVA WALILIA MAFUNZO,WATAKA WAFIKISHIWE VIJIJINI-KAGERA

Kibuka Prudence,Muleba(0756 872135)

BAADHI ya wamiliki wa vyombo vya moto wilayani Muleba mkoani Kagera,wameiomba serikali kuendeleza mafunzo ya muda fupi ya udereva ili kuepusha ajali zinazotokea mara kwa mara ambazo mara nyingi usababishwa na baadhi ya watumiaji wa vyombo hivyo kutojua sheria n a taratibu za uendeshaji.

Rai hiyo ilitolewa na wahitimu wa mafunzo ya awali ya udereva,katika risala iliyosomwa kwa niaba yao na bi.Prasidia Malinzi,ambapo zaidi ya wahitimu 100 kutoka kata za Kyebitembe,Karambi na Nshamba wilayani Muleba walihitimu mafunzo hayo na kutunukiwa vyeti na kaimu Kamanda wa jeshi la Polisi Vitus Mlolere,mwishoni mwa juma.

Madereva hao waliupongeza utaratibu wa kupeleka mafunzo vijijini, uliofanywa na jeshi la Polisi mkoani hapa kupitia kikosi cha usalama barabarani kwa kushirikiana na chuo cha mafunzo ya udereva cha Lake Zone Driving School cha mjini Bukoba.

Walisema kuwa kwa kipindi hiki ambapo jamii imekuwa na kasi katika manunuzi ya vyombo vya moto ambavyo ni pikipiki na magari,hakuna budi utaratibu huo ukaendelea ili kuelimisha watumiaji wa vyombo hivyo kwani wengi wanavitumia bila kujua sheria za udereva na usalama wao pia.

"Tunaomba elimu hii iendelee katika jamii yetu ili kuepusha ajali za mara kwa mara,tunaamini kwa kufanya hivi tutaepusha vifo vingi vinavyotokana na ajali"alisema Albogast Rushekya mmoja wa wahitimu wa mafunzo hayo.

Kwa upande wake mkurugenzi wa chuo cha udereva cha Lake Zone Driving School Winstone Kabantega,alisema mafunzo hayo yameendeshwa katika vituo viwili ndani ya wilaya ya Muleba ambavyo ni kata ya Kyebitembe na kata ya Nshamba,ambapo wahitimu wamejifunza kwa muda wa  siku tano,na tayari yamekuwa yakiendeshwa katika sehemu mbalimbali kulingana na wahitaji mara baada ya kuomba huduma hiyo.

Kabantega alisema kuwa mafunzo hayo yanaendeshwa kwa ushirikiano baina ya jeshi la Polisi mkoani Kagera na chuo cha Lake Zone Driving School,ambapo chuo kinatoa wakufunzi na jeshi la Polisi linatoa wataalamu kupia kikosi cha usalama barabarani.

Alisema kuwa moja ya malengo makuu ya mafunzo haya ni kuwafikishia wamiliki wa vyombo hivi mafunzo ya udereva popote pale wanapoona wanaweza kujipatia mafunzo ili kupunguza gharama ya kuyafuata katika vyuo ambavyo vinakuwa mbali na maeneo wanamoishi.

Aidha,Kabantega alisema kuwa mafunzo haya ni mwendelezo hasa baada ya kuwepo mabadiriko ya reseni ambavyo madereva wengi walikuwa nyuma kukidhi mahitaji ya kufuata utaratibu wa kujipatia reseni mpya.

Tuesday, May 1, 2012

MPENI SIFA NA KUTAMBUA MCHANGO WAKE,AKIWA HAI....

DK.MODEST RWABUBI,DAKTARI BINGWA NUSU KAFUTI MSTAAFU,anayemuunga mkono mkuu wa mkoa wa Kagera Kanali mstaafu Fabian Inyas Massawe,katika suala la usafi wa mazingira katika mjini wa Bukoba.

DAKTARI BINGWA RWABUBI,ambaye tayari amestaafu akiwa katika hosptali ya mkoa wa Kagera,amekuwa akijitolea katika shughuli mbalimbali za kijamii hasa kulingana na maeneo husika anamoishi.


Mojawapo ya kazi nzuri za kujitolea ni kuzibua mtaro korofi wa baraba ulioko katika barara ya Jamhuri(mbele ya Bohari kuu ya mkoa)Mtaro huu ulikuwa umeisha kuwa kero kwa wakazi wanaoishi katika maeneo hayo hususani wale wanaopangisha vyumba vya biashara katika jengo hilo la GPSA.

Wakati wa mvua,vyumba hivi vilikuwa vikifurika maji,na kuwalazimisha wapangaji kufanya kazi zao kwa shida kubwa,jambo ambalo kwa sasa linaonekana kutotokea mara baada ya mtaro huo kuzibuliwa na Dk.Rwabubi aliyeweka vijana kwa gharama zake ili kuepusha kero hiyo

Saturday, April 28, 2012

MJUE DAKTARI BINGWA MSTAAFU ANAYEJISHUGHULISHA NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA MJINI BUKOBA.....

Daktari Bingwa Nusu Kafuti Modest Rwabubi,Daktari mstaafu ambaye amejikita katika kuboresha kilimo cha mbogamboga ili kuhifadhi mazingira.
Jamii ya wanaopenda mboga za majani upendelea kufika kwa Daktari huyu kujipatia mboga za majani zisizo na kemikali au chumvichumvi,Daktari mstaafu anapatikana maeneo ya uvukweni karibu na Kiroyera tours.
Mojawapo ya shughuli anazoshughulika nazo Daktari huyu ni kuhiofadhi mazingira,hapa anashiriki katika kupanda mti kama ishara ya kuhifadhi mazingira katika ofisi ya Bohari ya mkoa Kagera,huku akiwa na Meneja aliyeamishiwa mkoani Arusha Bw.Ntaita.

Wednesday, April 4, 2012

TUWAPENI MOYO WANAOJITOKEZA KUCHANGIA MAENDELEO YA ELIMU NCHINI

KEMONDO,BUKOBA VIJIJINI

IMEELEZWA kuwa jamii kutokubali kuchangia kwenye suala la ujenzi wa vyumba vya madara,ni changamoto kuu inayochangia kishusha maendeleo ya kitaaluma kwa wanafunzi wa shule za sekondari wilayani Bukoba.

Hayo yalibainishwa na mkuu wa shule ya sekondari ya Kemondo Mwl.Charles Kalolora, iliyoko wilayani Bukoba mkoani Kagera,wakati wa hafla fupi ya kukabidhiwa vyumba vitano vya madarasa vilivyojengwa kwa nguvu ya ufadhiri kutoka wilayani humo.

Mwl.Karokola alisema kuwa jamii imekuwa ikisuasua katika michango ya ujenzi wa vyumba vya madarasa,na kusababisha watumishi wa shule kufanya kazi katika mazingira magumu jambo ambalo linachangia kurudisha maendeleo ya kitaaluma kwa wanafunzi.

Alisema maeneo mengi hali ya kukosa vyumba vya kufundishia ni kisababishi cha wanafunzi kushindwa kufanya vizuri katika mitihani yao,kwani kuwa na sehemu nzuri ya kufundishia ni sehemu inayochangia ufaulu wa wanafunzi katika mitihani yao ya mwaka.

Alisema kuwa shule hiyo pia,inakabiliwa na changamoto nyingine za muhimu kama vile kutokuwa na maabara kwa masomo ya sayansi,hali inayosababisha wanafunzi kushindwa kusoma kwa vitendo,kukosekana kwa maktaba pamoja na kutokuwa na walimu wa masomo ya hisabati na kiingereza.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya shule Bi.Mary Karega,alitoa rai kwa wakazi wa mkoa wa Kagera kutambua na kudhamini mchango mkubwa uliotolewa na wafadhili mbali kwa kukamilisha ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa.

Bi.Karega ambaye ni mkurugenzi wa kiwanda cha Mapanki kilicho kata ya Kemondo,alitoa pongezi kwa wafadhili hao kwa mchango wao mkubwa wa kutambua hitaji la elimu kwa jamii,na kuwataka majirani wengine wanaopenda maendeleo kuiga mfano wa wanajamii hao waliojitokeza kitoa msaada wao huo.

Alisema jamii imekuwa na mtazamo wa kwamba mfadhili lazima iwe taasisi kubwa,kumbe hata mtu mmoja mmoja anaweza kujitolea kujenga chumba cha darasa ikiwa ni sehemu ya mchango wake kwa jamii.

Aliwataja wafadhili walijitolea kufadhili ujenzi wa vyumba hivyo kuwa ni kampuni ya VicFish LTD iliyokamilisha ujenzi wa vyumba viwili,bw.Hamdan Suleiman,Kampuni ya Mapanki,bi.Saad Juma na Kemondo Ophans Care Center,ambao kila moja amejenga chumba kimoja kimoja kwa gharama ya shilingi 13.5 milioni kila chumba.

Katika taarifa ya meneja wa kampuni ya kusindika minofu ya samaki ya Vic Fish LTD iliyoko mjini Bukoba ilyosomwa kwa niaba yake na afisa utumishi wa kampuni Husein Buhuba,ujenzi wa vyumba hivyo umegharimu kiasi cha shilingi 23.5 milioni kupia mradi wa uvuvi endelevu,unaotekelezwa na kampuni hiyo.

Kwa upande wake meneja wa mradi wa uvuvi endelevu wa Vic Fish LTD,Jacob Maiseli,alisema msaada huo ni sehemu ya mradi kuangalia zaidi juu ya faida ya rasilimali za taifa inavyowasaidia wanajamii husika.Hivyo ni kujikita zaidi katika kurudisha fadhira kama sehemu ya kuendeleza jamii za wavuvi.

Maiseli alisema pamoja na kusaidia katika sekta ya elimu pia mradi huo unatekeleza katika mpango wa afya kwa kujenga vituo vya zahanati,kutoa huduma ya kiliniki kwa akina mama katika maeneo ya visiwani ambako ni Kerebe,Makibwa,Nyaburo,Nyabesige na Nyamukazi.

Alisema kuwa ufadhili wa vyumba viwili vya madarasa katika shule ya sekondari ya Kemondo umetokana na kuwepo na mwalo wa Rushara ambapo kiwanda cha Vic fish pia upokelea samaki kutoka kwa wavuvi hivyo ni jambo la muhimu kuchangia maendeleo ya eneo husika.